Tuesday, July 7, 2009

Mark 5

Mariko Ngovo - Mark 5

1.They went across the lake to the region of the Gerasenes.
Wakavuka across lake hadi wakafika ile area code ya Gerasenes.

2.When Jesus got out of the boat, a man with an evil spirit came from the tombs to meet him.
Wakati JC alidondoka kwa mv faina, mdhii fulani alikuwa na shaito ikimpossess alitoka makaburini akaishia kumkuta.

3.This man lived in the tombs, and no one could bind him any more, not even with a chain.
huyu msee aliishigi ndani ya makaburi, na wasee walikuwa washa sare kujaribu kumfunga, hata na chain.

4.For he had often been chained hand and foot, but he tore the chains apart and broke the irons on his feet. No one was strong enough to subdue him.
Ju nyakati mob alikuwa akitiwa chain kwa miguu na mikono lakini angeng'oa chain alafu angezivunja zile chuma walimfunga nazo miguu. Hakuna msee alikuwa ameshona enough kumfunga.

5.Night and day among the tombs and in the hills he would cry out and cut himself with stones.
Usiku na mchana angepiga manduru kwa makaburi na juu ya milima na kujikatakata na mawe.

6.When he saw Jesus from a distance, he ran and fell on his knees in front of him.
Wakati alicheki JC akikam toka mbali, alitoka mbio akaishia akamwangukia na magoti mbele yake.

7.He shouted at the top of his voice, "What do you want with me, Jesus, Son of the Most High God? Swear to God that you won't torture me!"
Akadai aki shout kwa voice yake yote,"Unanitakia nini, JC, mtoi wa Jah wa most high? Ebu swear na sir Godi hautani torture!"

8.For Jesus had said to him,"Come out of this man, you evil spirit!"
Ju JC alikuwa ashamshow,"Toka ndani ya huyo jamaa, we pepo wiked!"

9.Then Jesus asked him, "What is your name?" "My name is Legion," he replied, "for we are many."
Kisha JC akamshow niaje,"Jina yako ni nani?" mwenda akamshow,"jiina yangu ni Legion, ju si huoperate hapa wengi."

10.And he begged Jesus again and again not to send them out of the area.
Alafu akaomba JC tena na tena asiwatume nje ya hiyo hood.

11.A large herd of pigs was feeding on the nearby hillside.
Kulikuwa na mbuzi ulaya mob walikuwa wakisherehekea tu hapo ivo kando ya kilima.

12.The demons begged Jesus, "Send us among the pigs; allow us to go into them."
So pepo zikadai JC awagei perm, "Tutume kwa wale ma nguruwe; tukubalishe tuingie ndani ya hao ma pigs."

13.He gave them permission, and the evil spirits came out and went into the pigs. The herd, about two thousand in number, rushed down the steep bank into the lake and were drowned.
JC akawagei perm, hizo spirit wiked zikatoka nje ya huyo boy zikaingilia wale nguruwe. Iyo kundi yote ya nguruwe, kitu ka 2k, wakatoka teke wakafly over the cliff hadi ndani ya lake waka drown.

14.Those tending the pigs ran off and reported this in the town and countryside, and the people went out to see what had happened.
Wale wadhi walikuwa wanazichunga wakatoka unyoya wakaenda kutoa report ju ya hiyo storo ndani ya tao na mashambani, wadhii wakaishia kucheki what ilikuwa imehappen.

15.When they came to Jesus, they saw the man who had been possessed by the legion of demons, sitting there, dressed and in his right mind; and they were afraid.
Nyakati wakifika pale kwa JC, walicheki ule mse chizi mwenye alikuwa amepagawa na spirits wiked akiwa ametulia hapo, amedunga poa, ako normal; wakaingiza njeve.

16.Those who had seen it told the people what had happened to the demon-possessed man—and told about the pigs as well.
Wale walikuwa wamecheki hiyo drama yote walishow wasee chenye kilihappen kwa ule mzae mwenye alikuwa amepossessiwa na pia ju ya zile nguruwe.

17.Then the people began to plead with Jesus to leave their region.
Kisha wadhi wakaanza kuomba JC aishie toka kwa hood yao.

18.As Jesus was getting into the boat, the man who had been demon-possessed begged to go with him.
Sa nyakati JC akijitosa ndani ya na MV Faina, yule mse mwenye alikuwa amestruggle under hizo spirit wiked akadai aende na JC place JC alikuwa akiishia.

19.Jesus did not let him, but said, "Go home to your family and tell them how much the Lord has done for you, and how he has had mercy on you."
Lakini JC hangemkubali, akamshow."Ishia home kwa family yako na uwashow vile Sir
Godi amekudungia operation moja mezesha, na vile alikuonea huruma.

20.So the man went away and began to tell in the Decapolis how much Jesus had done for him. And all the people were amazed.
Basi yule mzeiya akaishia zake kwa zile miji kinde akaanza kutoa maelezo ya vile JC alikuwa amemduia mambo smart. Kila mdhii akashangaa.

21.When Jesus had again crossed over by boat to the other side of the lake, a large crowd gathered around him while he was by the lake.
Wakati JC alikuwa amevuka lake akiwa juu ya mv faina hadi ile ng'ambo ingine, rende bwaku ilijikusanya na kumzunguka akiwa kando ya lake.

22.Then one of the synagogue rulers, named Jairus, came there. Seeing Jesus, he fell at his feet.
Izo Nyakati mse; mmoja ya wale wadhi sonkwo wa hekalu, alikuwa anaitwa Jairus akatokezea hapo. Kucheki JC hivi, akadrop kwa miguu yake.

23.and pleaded earnestly with him, "My little daughter is dying. Please come and put your hands on her so that she will be healed and live."
akamshow tafadhal, "mtoi wangu dem ana die. Kam uwekelee mkono juu yake njo aget better aishi."

24.So Jesus went with him. A large crowd followed and pressed around him.
kwa ivo JC akaishia na yeye. Rende bwaku ilimfuata na kum bana hadi akashindwa kutembea.

25.And a woman was there who had been subject to bleeding for twelve years.
Alafu matha fulani mmoja aliukwa hapo mwenye alikuwa na shida ya damu ya miaka twelve.

26.She had suffered a great deal under the care of many doctors and had spent all she had, yet instead of getting better she grew worse.
Manze alikuwa ame go through vimeja tu sana akiishia kuchekiwa kila mara na madoki wengi, na alikuwa amepay bills zao hadi amesota, lakini instead ya kuwa better aliget worse.

27.When she heard about Jesus, she came up behind him in the crowd and touched his cloak,
Wakati aliskia kuhusu JC, alikam manyu yake ndani ya rendewalati ilikuwa imembana akaguza mbwenya yake.

28.because she thought, "If I just touch his clothes, I will be healed." Ju alifikiri,"Nikigusa tu kladi za huyu jamaa, nishakuwa sorted. Nitaget well."

29.Immediately her bleeding stopped and she felt in her body that she was freed from her suffering.
Mara one damu ikaacha kumwagika, akafeel ndani ya body yake ni ka ameget free toka iyo sickness.

30.At once Jesus realized that power had gone out from him. He turned around in the crowd and asked, "Who touched my clothes?"
Mara one JC pia naye ikam-hit haiya, kuna nguvu fulani imeflow nje yangu. Akageuka
akachek chek ndani ya rende akiuliza,"Nani aliguza kladi zangu?"

31."You see the people crowding against you," his disciples answered, "and yet you can ask, 'Who touched me?' "
Disciples wake wakashangaa akiuliza hivo hadi wakamshow niaje,"we unachekivile rende
inakubana, na bado unauliza ati naniameniguza?"
32.But Jesus kept looking around to see who had done it.
Lakini JC alizidi kucheki cheki aone niwho alikuwa ame do ivo.

33.Then the woman, knowing what had happened to her, came and fell at his feet and, trembling with fear, told him the whole truth.
Nyakati ule mshi alichekichenye kimemhappenia hadi ameget well, akakam akaanguka kwa
miguu ya JC na akishake ju ya kuingiza njeve akamshow ukweli yote.

34.He said to her, "Daughter, your faith has healed you. Go in peace and be freed from your suffering."
JC akamshowhuyo mshi,"Binti yangu, faith yako imekumake well. Ishia na amani na uwe free toka hiyo mashida."

35.While Jesus was still speaking, some men came from the house of Jairus, the synagogue ruler. "Your daughter is dead," they said. "Why bother the teacher any more?"
Nyakati JC akiongea bado, wadhi fulani walikam toka ile hao ya Jairus, yule sonkwo
aliongozaga hekalu, wakadai,"Binti yako amesha die, mbona usumbue mode tena?"

36.Ignoring what they said, Jesus told the synagogue ruler, "Don't be afraid; just believe."
JC akalenga chenye walikuwa wakisay, akashow huyo buda,"Usigwaye: we amini tu."

37.He did not let anyone follow him except Peter, James and John the brother of James.
Hakukubali mdhi mwingine amfuate except Pitaa, Jaymo na Johnie bro wa Jaymo.

38.When they came to the home of the synagogue ruler, Jesus saw a commotion, with people crying and wailing loudly.
Wakati walifika kwa ile keja ya buda sonkwo, JC akacheki ma commotion mob, wadhii wakipiga nduru na kutoa vilio loud.

39.He went in and said to them, "Why all this commotion and wailing? The child is not dead but asleep."
JC akacheck in alafu akawashow,"Mbona ma commotion mob na manduru? Mtoi si amelala tu!"

40.But they laughed at him. After he put them all out, he took the child's father and mother and the disciples who were with him, and went in where the child was.
Manze wadhiiwale wale wakamcheka deadly. Baada ya JC kuwachuja wote toka kwa hiyo hao, akachukua mbuyu wa mtoi na matha wa mtoi na wale wafuasi walikuw na yeye, akaishia ndani mahali mtoi alikuwa.

41.He took her by the hand and said to her, "Talitha koum!" (which means, "Little girl, I say to you, get up!" ).
Akashika mkono ya huyomtoi akamshow,"Talitha koum!" (inamaanisha,"Mtoi manzi msmall,
nakushow, amka!")

42.Immediately the girl stood up and walked around (she was twelve years old). At this they were completely astonished.
Mara moja manzi akarauka naakaanza kutembea tembea(alikuwa miaka twelve). Juu ya
hiyo drama, wote wakashtuka.

43.He gave strict orders not to let anyone know about this, and told them to give her something to eat.
JC akawagei order kali wasishow wasee ju ya hii stori, na alafu wagei mtoi dishi amange.

No comments:

Post a Comment