Saturday, October 31, 2009

Acts 1

Matendo ya masoja wa Jenerali JC!! Moja-Acts 1

1.In my former book, Theophilus, I wrote about all that Jesus began to do and to teach
Sa kwa mbuku ya mine, edition ya last kuchora, Buda Theo, nilichorea ju ya kila samo JC alianzisha ku do na ku teach

2.until the day he was taken up to heaven, after giving instructions through the Holy Spirit to the apostles he had chosen.
hadi mpaka vilee, vile alipokelewa majuu into heaven, of course baada ya kutoa ma instructions kupitia Holy Shpiri kwa ma apostles wenye alikuwa amechose.

3.After his suffering, he showed himself to these men and gave many convincing proofs that he was alive. He appeared to them over a period of forty days and spoke about the kingdom of God.
Baada ya ye ku-suffer, alijionyesha kwa hawa wadhii na akageiana proof mob za nguvu, za ku convince wadhii alikuwa alive. Aliwatokezea over period ya masiku forty na kuwazungumzia kuhusu kingdom ya sir Godi.

4.On one occasion, while he was eating with them, he gave them this command: "Do not leave Jerusalem, but wait for the gift my Father promised, which you have heard me speak about.
Time moja, vile alikuwa akidishi nao, aliwagei hii amri: "Msitoke from Jerusa, lakini tulieni
mkingoja gift yenyembuyuwangu wa heaven aliwapromise, yenye mmeskia nikibongajuu yake.

5.For John baptized with water, but in a few days you will be baptized with the Holy Spirit."
Ju Johnie alibaptize na wode, lakini siku kiasi tu zinakam mtabaptiziwa na the holy spirit."

6.So when they met together, they asked him, "Lord, are you at this time going to restore the kingdom to Israel?"
So vile walikutana pamoja, walimwuliza, "Bwana, ni we utahakikisha time hizi that kingdom
itarudi kwa Israel?"
7.He said to them: "It is not for you to know the times or dates the Father has set by his own authority.
Akawashow: "Sio for nyinyi kumesea the times ama the dates zenye mzae ameseti na his own authority.

8.But you will receive power when the Holy Spirit comes on you; and you will be my witnesses in Jerusalem, and in all Judea and Samaria, and to the ends of the earth."
Lakini mtapokea nguvu venye holy spirit atakam juu yenu; na mtakuwa mashahidi zangu Jerusa, hadi kwote Judea na Samaria, na hadi mwisho wa earth."
9.After he said this, he was taken up before their very eyes, and a cloud hid him from their sight.
Baada yake kubonga ivo, alikwachuliwa mbele ya macho yao live, na cloud ikamhide from sight.
10.They were looking intently up into the sky as he was going, when suddenly two men dressed in white stood beside them.
Walikuwa wamesimama ivo wakingethia juu na bidii kwa sky vile alikuwa akiishia,hapo hapo
suddenly tu wadhi wawili wamedunga white wakasimama kando yao.

11."Men of Galilee," they said, "why do you stand here looking into the sky? This same Jesus, who has been taken from you into heaven, will come back in the same way you have seen him go into heaven."
Wakanego aje,"Wadhi wa Galilee, mbona mnasimama hapa mkicheki sky ivo? Huyu huyu JC, mwenye amekwachuliwa from nyinyi hadi heaven, atarudi back style mmemcheki ameishia heaven."
12.Then they returned to Jerusalem from the hill called the Mount of Olives, a Sabbath day's walk from the city.
Kisha walirudi Jerusa toka hill inaitwa Mount Olives, place ilichukuaga sabbath mzima kufika na route 11.
13.When they arrived, they went upstairs to the room where they were staying. Those present were Peter, John, James and Andrew; Philip and Thomas, Bartholomew and Matthew; James son of Alphaeus and Simon the Zealot, and Judas son of James.
Vile walifika, waliishia upstairs hadi ile room place walikuwa wakitulia. Wale wadhi walikuwa hapo ilikuwa Peter, Johnie, Jaymo na Drew; Philo na Toma, Barthes na Marto; Jaymo mtoi son wa Alfie na Simo yule Jamaa wa chama cha maZealot,na Judee mtoi chali wa Jaymo.

14.They all joined together constantly in prayer, along with the women and Mary the mother of Jesus, and with his brothers.
Wote waka join pamoja wakiwa wamestand in prayer kila mara, wakiwa na ma mathe na Meri yule matha wa JC, na mabro wake.
15.In those days Peter stood up among the believers (a group numbering about a hundred and twenty)
Hizo siku Joh Pitaa alistand up katikati ya ma believers (rende ya wadhi kama soo moja na
twenty)

16.and said, "Brothers, the Scripture had to be fulfilled which the Holy Spirit spoke long ago through the mouth of David concerning Judas, who served as guide for those who arrested Jesus—
alafu akasema, "Ma bro niaje, ile scripture ili have kufulfilliwa yenye holy spiritalibonga
zamo kupitia mouth ya Davie ju ya Judee, mwenye alikuwa guide ya wale wadhii walishika JC-

17.he was one of our number and shared in this ministry."
alikuwa kwa namba yetu kama member na alishare hii huduma."
18.(With the reward he got for his wickedness, Judas bought a field; there he fell headlong, his body burst open and all his intestines spilled out.
(Lakini na ile munde ya zawadi yenye aliget ju ya vile alikuwa mwiked, Judee aliboti
shakee;hapo akafall flat body yake ika burst hadi matumbo zake zikatoka nje.

19.Everyone in Jerusalem heard about this, so they called that field in their language Akeldama, that is, Field of Blood.)
Kila mse Jerus aliskia hii stori,so waka call iyo shake na kilugha Akeldama, yaani, shakee ya
damu.)

20."For," said Peter, "it is written in the book of Psalms, " 'May his place be deserted;let there be no one to dwell in it,'and, " 'May another take his place of leadership.'
Pitaa akasema, "Ju imeandikwa ndani ya mbuku ya Psalms ati, 'wacha place yake isareiwe; wacha kusikuwe na mse wa kupoleaga hapo,' na, "Na mse mwengine akwachuplace yake ya uongozi.'

21.Therefore it is necessary to choose one of the men who have been with us the whole time the Lord Jesus went in and out among us,
Sasa ju ilikuwa necessary kuchose mmoja wa wale wadhi mwenye amekuwa na sisi time yote Bwana JC amepiga ma raundi kati yetu,

22.beginning from John's baptism to the time when Jesus was taken up from us. For one of these must become a witness with us of his resurrection."
kuanziaga ile matime ya baptism ya Johnie hadi ile time JC alikwachuliwa juu toka among sisi. Ju mmoja wa hao lazima akuwe witness na sisi wa kufufuka kwake."
23.So they proposed two men: Joseph called Barsabbas (also known as Justus) and Matthias.
So wakapropose wadhi wawili: Jose mwenye anaitwa Barsabbas (AKA Justus) na Matthias.

24.Then they prayed, "Lord, you know everyone's heart. Show us which of these two you have chosen
Kisha wakaomba, "Bwana, unamesea hearts za kila mtu.Tuonyeshe ni nani kati ya hawa wawili umesha chose

25.to take over this apostolic ministry, which Judas left to go where he belongs."
kutake over hii huduma ya ki apostle, yenye Judee aliacha ku go place yenye anabelong."

26.Then they cast lots, and the lot fell to Matthias; so he was added to the eleven apostles.
Kisha waka cast ma lots na dice ikachagua Matthias; kwa ivo akaongezwa kwa wadhii ma apostles eleven.

Saturday, October 24, 2009

John 21

Johnie twenty 0ne - John 21

1.Afterward Jesus appeared again to his disciples, by the Sea of Tiberias.It happened this way:
Tena bahadayez Jesus akatokezea wafuasi wake, kando ya sea ya Tiberias. Ili happen ivi:

2.Simon Peter, Thomas (called Didymus), Nathanael from Cana in Galilee, the sons of Zebedee, and two other disciples were together.
Simon Peter, Thomas AKA Didymus, Nathaniel yule wa Cana ya Galilee, wale sons Zebedayo na wafuasi mbe wengine walikuwa tugezza.

3."I'm going out to fish," Simon Peter told them, and they said, "We'll go with you." So they went out and got into the boat, but that night they caught nothing.
Simon Peter akawashow, "Mi naishia out kufish." Wakamshow,"tutaishia na wewe." Kwa ivo wakaishia out wakapanda boat, lakini hiyo night hawakushika anything.

4.Early in the morning, Jesus stood on the shore, but the disciples did not realize that it was Jesus.
Ngware asubuhi, JC akasimama kwa ufuo, lakini wale wafuasi hawakumesea that ilikuwa Jesus.

5.He called out to them, "Friends, haven't you any fish?" "No," they answered.
Akawaita kuwauliza, "Majamaa, hamna any fish?" "Wakamshow, "zi."

6.He said, "Throw your net on the right side of the boat and you will find some." When they did, they were unable to haul the net in because of the large number of fish.
Akasema, "Tupeni net kwasideya right ya boat na mtaget kadhaa." Vile walitupa neti,walishindwa kuchomoa net kwa maji kuweka kwa boat ju ya vile walishika samaki mob.


7.Then the disciple whom Jesus loved said to Peter, "It is the Lord!" As soon as Simon Peter heard him say, "It is the Lord," he wrapped his outer garment around him (for he had taken it off) and jumped into the water.
Kisha yule mfuasi mwenye JC alipenda akashow Peter, "Nibwana mdosi!" Vile tuSimon Peter aliskia akisema, "Ni bwana mdosi,"akajifunga nguo yake ya nje (Ju alikwa ameivua) akaruka ndani ya maji.

8.The other disciples followed in the boat, towing the net full of fish, for they were not far from shore, about a hundred yards.
Wale wafuasi wengine wakafuatilia wakiwa ndani ya boat, wakivuta ile net imeshona ma fish, ju hawakuwa far na ufuo, kedo ninety meters.

9.When they landed, they saw a fire of burning coals there with fish on it, and some bread.
Vile waliland, wakacheki nare ya makaa hapo, ka barbeque kafish juu yake, na dibre kiasi.

10.Jesus said to them, "Bring some of the fish you have just caught."
JC akawashow niaje, "Ebu leteni fish kiasi hapo kwa zenye mmeshika tu saa hii."

11.Simon Peter climbed aboard and dragged the net ashore. It was full of large fish, 153, but even with so many the net was not torn.
Simon Peter akapanda juu ya boat akakokota net hadi kwa ufuo. Ilikuwa imeshona samaki wa soo ka, 153, lakini bado na fish mob hivo haikuraruka.

12.Jesus said to them, "Come and have breakfast." None of the disciples dared ask him, "Who are you?" They knew it was the Lord.
JC akawashow,"Kamini mjitibu ka breako." Hanaku hata disciple mmoja mwenye alimwuliza, "We njo nani?" Walimesea ilikuwa JC.

13.Jesus came, took the bread and gave it to them, and did the same with the fish.
JC akakam akakwachu ile loaf akawagei, alafuaka do ivo ivo na ile fish.

14.This was now the third time Jesus appeared to his disciples after he was raised from the dead.
Sa hii ilikuwa mara ya tatu JC ali tokezea kwa wafuasi wake after akuwe raised from the dead.

15.When they had finished eating, Jesus said to Simon Peter, "Simon son of John, do you truly love me more than these?" "Yes, Lord," he said, "you know that I love you." Jesus said, "Feed my lambs."
Vile walikuwa wamemada kudishi, JC akabongesha Simon Peter kumshow, "Simo mtoi wa Johnie, for real unanipenda ukweli kuliko hivi?" Peter akamshow, "Ndio bwana mdosi, unamesea nakupenda." JC akamshow, "Feed Kondoo za mine."

16. Again Jesus said, "Simon son of John, do you truly love me?" He answered, "Yes, Lord, you know that I love you." Jesus said, "Take care of my sheep."
Tena JC akasema, "Simomtoi wa Johnie, kwani unanipenda for real? Akamjibu, "Eeh, bwana mdosi, unamesea that nakupenda." JC akamshow, "Chunga kondoo zangu."

17. The third time he said to him, "Simon son of John, do you love me?" Peter was hurt because Jesus asked him the third time, "Do you love me?" He said, "Lord, you know all things; you know that I love you."Jesus said, "Feed my sheep.
Ile time ya tatu akamshow,"simo mtoi wa Johnie, unanipenda?" Peter akakuwa hurt ju JC alimwuliza mara ya tatu, "Je unanipenda?" Akasema, "Lord, unamesea kila kitu; unajua nakupenda." JC akamshow, Feed kondoo za mine."

18 I tell you the truth, when you were younger you dressed yourself and went where you wanted; but when you are old you will stretch out your hands, and someone else will dress you and lead you where you do not want to go."
Nakushow ukweli, vile ulikuwaga yankee ulijivalisha mwenyewe na kuishia ile place ulitaka; lakini vile utakuwa mu old utastretch out mkono yako, na mse mwengine atakuvalisha kladina kukulead ile place hautaki kuishia."

19Jesus said this to indicate the kind of death by which Peter would glorify God. Then he said to him, "Follow me!"
Jesus akasema ivo kuwashow ile kind ya kudedi by which Peter ange glorify sir Godi.Kisha
akamshow niaje, "Nifuate!"

20.Peter turned and saw that the disciple whom Jesus loved was following them. (This was the one who had leaned back against Jesus at the supper and had said, "Lord, who is going to betray you?")
Peter akageuka akacheki yule disciple mwenye JC alipenda akiwafuata. (Huyu alikuwa yule jamaa mwenye alikuwa ame leanback akilalia JC ile time ya supper na alikuwa amedai, "Bwana mdosi, nana anaenda kuku betray?")

21.When Peter saw him, he asked, "Lord, what about him?"
Vile Peter alimcheki, aliuliza, "Bwana mdosi, na je, what about huyu jamaa?"

22.Jesus answered, "If I want him to remain alive until I return, what is that to you? You must follow me."
JC akamjibu, ""Kama na want abaki alive hadi nirudi, hiyo ni nini kwako? Nimust unifuate."

23.Because of this, the rumor spread among the brothers that this disciple would not die. But Jesus did not say that he would not die; he only said, "If I want him to remain alive until I return, what is that to you?"
Ju ya this, fununu ika spread among ma bros ati huyu disciple hange dedi. lakini JC hakusema
ati hangededi; alisema tu ati, "Kama na want abaki alive hadi nirudi, hiyo ni nini kwako?"

24.This is the disciple who testifies to these things and who wrote them down. We know that his testimony is true.
Huyu njo yule disciple mwenye anashuhudia ju ya hizi vitu na mwenye alizi write down. Tunamesea kuwa ushahidi wake ni ukweli.

25.Jesus did many other things as well. If every one of them were written down, I suppose that even the whole world would not have room for the books that would be written.
JC akado vitu zingine mob pia. Ka kila moja ya zote ingeaandikwa down, nadhani hata world nzima haingekuwa na room za kutosha for zile books zingeandikwa.

Monday, October 19, 2009

John 20

Johnie Chapta Blue - John 20


1.Early on the first day of the week, while it was still dark, Mary Magdalene went to the tomb and saw that the stone had been removed from the entrance.
Ngware na mapema, siku ya fao ya wiki, vile kulikuwa bado giza, Mary Magda aliishia kwa grave na kucheki ivi akakuta jiwe imesongeshwa from mlango ya grave.


2.So she came running to Simon Peter and the other disciple, the one Jesus loved, and said, "They have taken the Lord out of the tomb, and we don't know where they have put him!"
Kwa ivo akaishia unyoya hadi kwa Simo yani Peter na yule disciple mwingine, mwenye JC alipenda, na kudai, "Wamesha kwachu bwana mdosi toka kwa tomb, na hatushikanishi ni wapi wanaweza kuwa wamemweka!"


3.So Peter and the other disciple started for the tomb.
Kwaivo Pitaa na yule jamaa mwingine disciple wakaelekea kwa kaburi.


4.Both were running, but the other disciple outran Peter and reached the tomb first.
Wote walikuwa masaa wanahepa mbio, lakini yule mfuasi mwingine akahepa spidi kuliko Pitaa akafika kwa kaburi wa first.


5.He bent over and looked in at the strips of linen lying there but did not go in.
Akainama over na kupeep ndani kucheki zile vitambaa za khaki zilikuwa zimewachwa hapo lakini hakuingia ndani.


6.Then Simon Peter, who was behind him, arrived and went into the tomb. He saw the strips of linen lying there,
Kisha Pitaa yani Simo, mwenye alikuwanyuma yake akafika nakuingia ndani ya kaburi. Alicheki zile vitambara zimelala hapo,


7.as well as the burial cloth that had been around Jesus' head. The cloth was folded up by itself, separate from the linen.
tugezza na ile kitambaa ya kuzikia yenye ilikuwa imecover around kichwa ya JC. Iyo kitambaa ilikuwa imefungwa pekee, iko separate from ilekhaki.


8.Finally the other disciple, who had reached the tomb first, also went inside. He saw and believed.
Finally yuledisciple mwingine, mwenyealifika wa faokwa kaburi, pia akaingia ndani. Akacheki mwenyewe halafu akaamini.


9.(They still did not understand from Scripture that Jesus had to rise from the dead.)
(Bado hawakuelewa from scriptures that ilimbidi JC a rise toka kwa the dead.)


10.Then the disciples went back to their homes,
Kisha wale wafuasi wakarudi back hadi kwa ma home zao,


11.but Mary stood outside the tomb crying. As she wept, she bent over to look into the tomb
lakini Mary alisimama nje ya kaburi akilia. Vile alikuwa akiweep, akainama over kuchungulia
ndani ya kaburi


12.and saw two angels in white, seated where Jesus' body had been, one at the head and the other at the foot.
alafu akacheki angels mbe in white, wamepolea place mwili ya JC ilikuwaga bafore, mmoja kwa place ya kichwa namwingine kwa place miguu zilikuwa.


13.They asked her, "Woman, why are you crying?" "They have taken my Lord away," she said, "and I don't know where they have put him."
Wakauliza madam, "Mama, mbona unalia?" Matha akawashow, "Wamechukua bwana mdosi wangu away, na simesei ni wapi wamemweka."


14.At this, she turned around and saw Jesus standing there, but she did not realize that it was Jesus.
Kufika hapo, aka turn around akacheki JC amesimama hapo,lakini hakurealize ilikuwa JC.


15."Woman," he said, "why are you crying? Who is it you are looking for?" Thinking he was the gardener, she said, "Sir, if you have carried him away, tell me where you have put him, and I will get him."
Jesus akamwuliza, "Mama, mbona umeangua kilio? Unasaka nani?" Madam, akifikiria ni shamba boy akadai, "Boss, kama ni wewe umemchukua away nishow place umemweka, nitamget."


16.Jesus said to her, "Mary."She turned toward him and cried out in Aramaic, "Rabboni!" (which means Teacher).
JC akamjibu madam, "Mary." Madam akageuka toward JC na kuwika na ki Aramaic, "Rabboni!" (word yenye hu mean Odijo).


17.Jesus said, "Do not hold on to me, for I have not yet returned to the Father. Go instead to my brothers and tell them, 'I am returning to my Father and your Father, to my God and your God.' "
JC akamshow, "Usinikwamilie, ju bado sijarudi yet kwa Mbuyu. Ishia instead hadi kwa bros zangu uwashow, 'Ninarudi kwa mbuyu wanguna mbuyuwenu, kwa sir godi wangu na sir Godi wenu.' "


18.Mary Magdalene went to the disciples with the news: "I have seen the Lord!" And she told them that he had said these things to her.
Mary Magda akaishia kwa wafuasi wake nahabari: "Nimecheki bwana mdosi!" Na alafu akawashow kuwa JC alikuwa amebonga zile vitu zote kwake.


19.On the evening of that first day of the week, when the disciples were together, with the doors locked for fear of the Jews, Jesus came and stood among them and said, "Peace be with you!"
Ile jioni yathat first day ya wiki, vile wafuasi walikuwa pamoja,na doaa zimefungwa ju ya
kugwaya cos of the jews, JCalikam akasimama among the nakuwashow, "Peace iwe na nyinyi!"


20.After he said this, he showed them his hands and side. The disciples were overjoyed when they saw the Lord.
After alikuwa amesema hivi, aliwashow mikono zake na sideyake. ma disciples walikuwa overjoyed vilewalicheki bwana mdosi.

21.Again Jesus said, "Peace be with you! As the Father has sent me, I am sending you."
Tena JC akasema, "Peace ikuwe na nyinyi! Vile mbuyuamenituma pia nawatuma."


22.And with that he breathed on them and said, "Receive the Holy Spirit.
Na with that akawabreathia na kusema, "Receive-ini Holy Spirit.


23.If you forgive anyone his sins, they are forgiven; if you do not forgive them, they are not forgiven."
Mki forgive mse yeyote dhambi zake, wameforgiviwa; msipowasamehea, hawajasamehewa."


24.Now Thomas (called Didymus), one of the Twelve, was not with the disciples when Jesus came.
Sa Thomas mwenye pia alimeseka ka Didymus, mmoja wa wale twelve, hakuwa na disciples wenzake vile JC alikam.


25.So the other disciples told him, "We have seen the Lord!" But he said to them, "Unless I see the nail marks in his hands and put my finger where the nails were, and put my hand into his side, I will not believe it."
Kwa ivo wale wafuasi wengine wakamshow niaje, "Tumeshacheki bwana mdosi!" Lakini akawashow, "Unless nicheki zile marks za misumari kwa mikono zake,na niweke kidole yangu place nails zilikuwa,na niweke mkono yangu kwa side yake, sita believe."


26.A week later his disciples were in the house again, and Thomas was with them. Though the doors were locked, Jesus came and stood among them and said, "Peace be with you!"
Wiki moja later wafuasi wake walikuwa ndani yambanyu tena,na Thomas alikuwa nao. Ingawa ma doaa zilikuwa locked, JC alikam akasimama kati yao nakuwashow, "Peace iwe na nyinyi!"


27.Then he said to Thomas, "Put your finger here; see my hands. Reach out your hand and put it into my side. Stop doubting and believe."
Kishakashow Thomas, "Wekelea kidole yako hapa; cheki mikono zangu. Direct mkono yako na uiwekendani ya sideyangu. Wacha ku doubt na uamini.


28.Thomas said to him, "My Lord and my God!"
Thomas akamshow, "bwana mdosi wangu na sir Godi wangu!"


29.Then Jesus told him, "Because you have seen me, you have believed; blessed are those who have not seen and yet have believed."
Kisha JC akamshow niaje, "Ju umenicheki,umeamini; wameblessika wote wenye hawajanicheki lakini wameamini."


30.Jesus did many other miraculous signs in the presence of his disciples, which are not recorded in this book.
JC ali do signs mob miraculousmbele ya wafuasi wake, zenye hazijaandikwa kwa hii book.


31But these are written that you may believe that Jesus is the Christ, the Son of God, and that by believing you may have life in his name.
Lakini hizi vitu zimeandikwa njo muamini that JC njo kristo, son wa sir Godi, na that by ku
believe mtakuwana uhai in jina yake.

Friday, October 16, 2009

John 19

Johnie Chapta ya nineteen-John 19

1.Then Pilate took Jesus and had him flogged.
Alafu Pilate akakwachu Jesus akamsare kuwashwa viboko.

2.The soldiers twisted together a crown of thorns and put it on his head. They clothed him in a purple robe
Masoja wakakunja kunja tugezza ka crown ka miba wakamwekea kwa head yake. Wakamvalisha clad fulani, robe, ya purple

3.and went up to him again and again, saying, "Hail, king of the Jews!" And they struck him in the face.
Alafu wakaishia kwake tena na tena wakimshow, "Oyee, king wa ma jews!" Na wakamwai vibare za uso.

4.Once more Pilate came out and said to the Jews, "Look, I am bringing him out to you to let you know that I find no basis for a charge against him."
Maraingine tena Pilate akakam nje kubongesha wayahudi niaje,"Chekini, nalete JC nje kwenu njo niwafanye mumesee that sioni beef ina warrant mu press charges against yeye."

5.When Jesus came out wearing the crown of thorns and the purple robe, Pilate said to them, "Here is the man!"
Vile JC alitokezea amevalishwa crown ya ma miiba na kabuti yapurple, Pilate akawabongesha, "Huyu hapa huyo jamaa!"

6.As soon as the chief priests and their officials saw him, they shouted, "Crucify! Crucify!" But Pilate answered, "You take him and crucify him. As for me, I find no basis for a charge against him."
Vile tu ma priest sonkwo na ma officiale walimcheki, wakaanza kuwika tena,"Mcrucify! mcrucify!" Lakini akawajibu niaje, "mchukueni mkamcrucify. Lakini for mimi, sioni beef yoyote ya kuleta such charges against JC."

7.The Jews insisted, "We have a law, and according to that law he must die, because he claimed to be the Son of God."
Wale wayahudi wakadai niaje, "Tuko na constitution wajamaa, na kulingana na constitution yetu lazima amadwe, ju alidai ye ni son wa sir Godi."

8.When Pilate heard this, he was even more afraid,
Weh!Pilate kuskizia hizo latest developments akaingiza mnjeve sa ile zaidi,

9.and he went back inside the palace. "Where do you come from?" he asked Jesus, but Jesus gave him no answer.
akaishia ndani ya palace tena. "Unatokezea wapi jamaa?" Akauliza Jesus, lakini Jesus akakwara kumjibu.

10."Do you refuse to speak to me?" Pilate said. "Don't you realize I have power either to free you or to crucify you?"
Pilate akamshow niaje, "Unakwara kubongana mimi? Haumesei niko na powers za either kukufree ama kukucrucify kwa cross?"

11.Jesus answered, "You would have no power over me if it were not given to you from above. Therefore the one who handed me over to you is guilty of a greater sin."
JC akamjibu mara one, "Haungekuwa na powers ju ya mimi ka hazingekuwa zilipeanwa kwako toka mbinguni.Kwa hivo ju ya hiyo stori yule jamaa alinisare kwako ako guilty ju ya dhambi bwaku zaidi."

12.From then on, Pilate tried to set Jesus free, but the Jews kept shouting, "If you let this man go, you are no friend of Caesar. Anyone who claims to be a king opposes Caesar."
Toka hapo sa, Pilate akatry kumwachilia JC as a free jamaa, lajkini wayahudi mtu wangu, wayahudi walibaki kuwika tu, "Ukiset huyujamaa free aishie tu, we basi sio beshte wa Caesar. Ju kila mse anadai ye ni king analeta compe kwa Caesar."

13.When Pilate heard this, he brought Jesus out and sat down on the judge's seat at a place known as the Stone Pavement (which in Aramaic is Gabbatha).
Vile Pilate aliskia hiyo siasa mbaya, alileta JC nje akapolea kwa kiti ya judge place ilijulikana ka pevu ya stone (In aramaic inameseka ka Gabbatha).

14.It was the day of Preparation of Passover Week, about the sixth hour."Here is your king," Pilate said to the Jews.
Ilikuwaga ile day ya preps za passover week, kitu ka masaa sita ivi. Pilate akaanza kubonga, "Njo huyu king wenu."

15.But they shouted, "Take him away! Take him away! Crucify him!" "Shall I crucify your king?" Pilate asked."We have no king but Caesar," the chief priests answered.
Lakini vile walishout, "Matake-ini away! Mtake-ini away! Mcrucifyini!" Pilate akauliza niaje, "Kwani nita crucify King wenu?" Ma priests wasonkwo wakasema, "Si hatuna king except Caesar."

16.Finally Pilate handed him over to them to be crucified. So the soldiers took charge of Jesus.
Mwishowe Pilate akamsare over kwa wayahudi wam crucify. Kwa ivo masoja waka chukua charge over JC.
17.Carrying his own cross, he went out to the place of the Skull (which in Aramaic is called Golgotha).
Akibeba cross yake mwenyewe, wakaishia out hadi wakafika ile place ya skull (penye in aramaic inaitwaga Golgotha).

18.Here they crucified him, and with him two others—one on each side and Jesus in the middle.
Hapo wakam crucify, yeye pamoja wasee wengine waili madingo-mmoja kwa side yake ya left na mwingine kwa side yake ya right na JC katikati.

19.Pilate had a notice prepared and fastened to the cross. It read: JESUS OF NAZARETH, THE KING OF THE JEWS.
Pilate aka-order notice imake-iwe akaichapilia kwa cross. Ilisoma: Jesus wa Nazareth, King wa Jews.

20.Many of the Jews read this sign, for the place where Jesus was crucified was near the city, and the sign was written in Aramaic, Latin and Greek.
Wengi wa wayahudi walisoma hiyo lebo, ju ile place yenye JC alikuwa amecrucifyiwa ilikuwa karibu ya jiji, na notice ilikuwa imeandikwa na Aramaic, Latin na greek.

21.The chief priests of the Jews protested to Pilate, "Do not write 'The King of the Jews,' but that this man claimed to be king of the Jews."
Yule mdosi wa ma pasii wa kiyahudi alicomplain kwa Pilate,"Usiandike ati, 'King wa wayahudi,' lakini that huyu jamaa alidai kuwa 'King wa the Jews."
22.Pilate answered, "What I have written, I have written."
Pilate akasema, "Chenye nimechora, nimechora."

23.When the soldiers crucified Jesus, they took his clothes, dividing them into four shares, one for each of them, with the undergarment remaining. This garment was seamless, woven in one piece from top to bottom.
Vile wale masoja walicrucify JC, walikwachu cladi zake, wakazigawanya kwa vipande nne, moja ya kila mmoja wao, na ile underwear ikibakishwa. Underwear ilikuwa kitambaa moja tu haina hem, imeshonwa ka kipande kimoja from juu hadi down.

24."Let's not tear it," they said to one another. "Let's decide by lot who will get it."
This happened that the scripture might be fulfilled which said,"They divided my garments among them and cast lots for my clothing." So this is what the soldiers did.
Wakareason aje wakiwa together, "Tusiirarue. Tu decide na coin ni nani ataiget." Hii ilihapen njo scripture ikuwe fulfilled yenye husema, "Walidivide clothes zangu kati yao na kutoss coin ju ya kladi zangu." So ivo njo masoja walido.

25.Near the cross of Jesus stood his mother, his mother's sister, Mary the wife of Clopas, and Mary Magdalene.
Karibu tu ya cross ya Jesus,kulikuwa na mathaake, siz wa mathaake, Merii waif wa Clopas na Mary Magdalne wamesimama hapo.

26.When Jesus saw his mother there, and the disciple whom he loved standing nearby, he said to his mother, "Dear woman, here is your son,"
Vile JC alicheki mathaake amestand pale, na disciples wake mwenye alilike amesimama hapo karibu, alishow mathaake, "Mama mpendwa, njo huyu son wako,"

27.and to the disciple, "Here is your mother." From that time on, this disciple took her into his home.
na kwa yule mfuasi, "Huyu njo mathaako." Toka hiyo time kuendelea, disciple wake akamchukua matha wa JC na wakaishi kwake.


28.Later, knowing that all was now completed, and so that the Scripture would be fulfilled, Jesus said, "I am thirsty."
Bahadayez, akimesea kila something ilikuwa imemalizika, na pia njo scripture ika kuwa kweli, JC akasema, "Niko thirsty."

29.A jar of wine vinegar was there, so they soaked a sponge in it, put the sponge on a stalk of the hyssop plant, and lifted it to Jesus' lips.
Chupa ya wine imesha chacha kuwa vinegar ilikuwa hapo, wakatumbukiza sponge ndani, wakawekelea sponge kwa kijiti ya plant inaitwa hyssop wakaiinua hadi kwa lips za JC.

30.When he had received the drink, Jesus said, "It is finished." With that, he bowed his head and gave up his spirit.
Vile alimada kukwachu drink, Jesus akasema, "Imekwisha kukwisha."Na with that, aka bow head na kuasare spirit yake.

31.Now it was the day of Preparation, and the next day was to be a special Sabbath. Because the Jews did not want the bodies left on the crosses during the Sabbath, they asked Pilate to have the legs broken and the bodies taken down.
Sa ilikuwa ni siku ya preps, na ile day next njo ilikuwa ikuwe sabbath ile special. Ju wayahudi
hawakutaka bodies zao zibaki kwa cross during sabbath, waliuliza Pilate atumane masoja wavunje miguu za wale wadhi na bodies zao zishukishwe down.

32.The soldiers therefore came and broke the legs of the first man who had been crucified with Jesus, and then those of the other.
Wale mabanga wakakam wakavunja miguu za dingo wa fao mwenyealikuwaamecrucifyiwa na pamoja JC, alafu pia wakavunja za dingo wa pili.

33.But when they came to Jesus and found that he was already dead, they did not break his legs.
Lakini vile walikam kwa JC na kukuta asha kick, hawaku break miguu zake.
34.Instead, one of the soldiers pierced Jesus' side with a spear, bringing a sudden flow of blood and water.
Instead mmoja wao mabanga alimdunga JC kwa side na spear, ikaleta flow ya blood na wode vi sudden.

35.The man who saw it has given testimony, and his testimony is true. He knows that he tells the truth, and he testifies so that you also may believe.
Yule jamaa alicheki hii drama alipeana ushahidi, na testimony yake ni ukweli.Anamesea that anabonga ukweli, na anatestify njo hata nyi muamini.

36.These things happened so that the scripture would be fulfilled: "Not one of his bones will be broken,"
Hizi vitu zilihappen njo scripture itimike: "Hata mmoja ya bones zake haitavunjika,"

37.and, as another scripture says, "They will look on the one they have pierced."
na, scripture ingine inasay, "Watacheki yule jamaa mwenye walidunga."
38.Later, Joseph of Arimathea asked Pilate for the body of Jesus. Now Joseph was a disciple of Jesus, but secretly because he feared the Jews. With Pilate's permission, he came and took the body away.
Baadaye, Josewa arimathea akauliza Pilate amgei mwili ya JC. Sa Jose alikuwa disciple wa JC, lakini ki clande ju aliogopa wayahudi. Na perm ya Pilate, akakam akakwachu mwili ya JC akaishia nayo.

39.He was accompanied by Nicodemus, the man who earlier had visited Jesus at night. Nicodemus brought a mixture of myrrh and aloes, about seventy-five pounds.
Nicodemus alikuwa amemzindii yule jamaa, Nicodemus mwenye mapema kidogo alikuwa amevisit JC usiku.
Nico alileta mix ya myrrh na aloe vera,kilo kama thirty five.

40.Taking Jesus' body, the two of them wrapped it, with the spices, in strips of linen. This was in accordance with Jewish burial customs.
Wakikwachu mwili ya JC, hao wadhi mbe waliifunikia, wakiwa wameipaka ma spices, nadni ya vitambaa za khaki. Hiyo ilikuwa kulinganana traditions za wayahudi.

41.At the place where Jesus was crucified, there was a garden, and in the garden a new tomb, in which no one had ever been laid.
Kwa ile placeJC alikuwa amecrucifyiwa, kulikuwa na shakee, na ndani ya shakee kulikuwa na kaburi mbichi, yenye hanaku msealikuwa amezikwa ndani.

42.Because it was the Jewish day of Preparation and since the tomb was nearby, they laid Jesus there.
Ju ilikuwa ni siku ya ma jews siku ya preps na ju kulikuwa na kaburi hapo close by, walilaza JC hapo.

Tuesday, October 13, 2009

John 18

Johnie Chapta ya eighteen -John 18


1.When he had finished praying, Jesus left with his disciples and crossed the Kidron Valley. On the other side there was an olive grove, and he and his disciples went into it.
Vile alimada kusali, Jesus akakitoa pamoja na wafuasi na ku cross kidron ile valley. Ile ngambo ingine, abroad, kulikuwa na kichaka cha ma olives, na hapo JC na wafuasi wakajichoma ndani.

2.Now Judas, who betrayed him, knew the place, because Jesus had often met there with his disciples.
Sa Judee, mwenyealimwuza, alimesea ile place, ju JC alikuwaga mara most akiishia kumeet hapo na wafuasi.

3.So Judas came to the grove, guiding a detachment of soldiers and some officials from the chief priests and Pharisees. They were carrying torches, lanterns and weapons.
Kwa ivo Judee akasogelea kichaka, akiguide unit moja ja mabanga pamoja na wadosi fulani toka kwa mapriest sonkwo na mafarisayo. Walikuwa wakibeba torch na koroboi na ma weapons.
4.Jesus, knowing all that was going to happen to him, went out and asked them, "Who is it you want?"
JC ju alimesea kila kitu chenye kilikuwa kinaenda kuhappen kwake, aliishia nje na kudai,"Ni nani mna want?"

5."Jesus of Nazareth," they replied.
"I am he," Jesus said. (And Judas the traitor was standing there with them.)
"JC mse wa Nazareth," wakamshow. JC akawashow, "Mi njo yeye." (Judee mwuzaji alikuwa amesimama apo nao)

6.When Jesus said, "I am he," they drew back and fell to the ground.
Vile JC alisema, "Mi njo yeye," wakarudi nyuma na kudundakwa grao.

7.Again he asked them, "Who is it you want?" And they said, "Jesus of Nazareth."
Kisha tena akawauliza niaje, "Ni nani mnawant?" Waadai tena, "Jesus yule wa Nazareth."

8."I told you that I am he," Jesus answered. "If you are looking for me, then let these men go."
JC akawareplyia, "Nimewashow mi njo yeye. Ka mnanisaka basi achaneni na hawa wadhii wakiteme."

9.This happened so that the words he had spoken would be fulfilled: "I have not lost one of those you gave me."
Hi ilihappen njo zile words alikuwa amebonga zingefulfillika: "Sijalostisha hata mmoja wa wale ulinigei."

10.Then Simon Peter, who had a sword, drew it and struck the high priest's servant, cutting off his right ear.(The sevrvant's name was Malchus.)
The Kisha Simo yule pitaa, mwenye alikuwa na njora, akaichomoa na kumwai mboch mmoja hapo ivo alikuwaga servant wa high priest, akakata skio yake ya right(Jina ya huyo mboch ilikuwa Malchus.)

11.Jesus commanded Peter, "Put your sword away! Shall I not drink the cup the Father has given me?"
Jesus akacommand Pitaa, "Ebu weka njora yako away! Kwani sitakunywa ile cup mbuyuz amenigei?"

12.Then the detachment of soldiers with its commander and the Jewish officials arrested Jesus. They bound him
Kisha ile unit ya mabanga pamoja na OCPD wao na wale wadosi wayahudi waka arrest JC. Wakamfunga

13.and brought him first to Annas, who was the father-in-law of Caiaphas, the high priest that year.
wakamleta place ya fao kwa Annas, yule jamaa alikuwa fadhein law wa Caiaphas, high priest sasa wa hiyo mwaka.

14.Caiaphas was the one who had advised the Jews that it would be good if one man died for the people.
Caiaphas alikuwaga the one mwenye alikuwa amedunga wayahudi advise that ingekuwa poa ka mse mmoja ange die for wadhii.

15.Simon Peter and another disciple were following Jesus. Because this disciple was known to the high priest, he went with Jesus into the high priest's courtyard,
Simo yule Pitaa na mfuasi mwingine walikuwa wakifuata JC bumper. Ju huyu mfuasi alikuwa anajulikana kwa high priest, aliingia na JC hadi kwa verandah za high priest,

16.but Peter had to wait outside at the door. The other disciple, who was known to the high priest, came back, spoke to the girl on duty there and brought Peter in.
lakini Pitaa ikabidi amekabaki amengoja kwa doaa. Yule mfuasi celeb, mwenye alimeseka na high priest akarejelea, akanego na dem alikuwa duty iyo time wakaingiza Pitaa ndani.
17."You are not one of his disciples, are you?" the girl at the door asked Peter.
He replied, "I am not."
Yule dem alikuwa kwa doaa akahoji Peter,"We sio mmoja wa wahaudi sio, ama we ni member?" Jamaa akajibu, Zii, mi si member jo!"
18.It was cold, and the servants and officials stood around a fire they had made to keep warm. Peter also was standing with them, warming himself.
Ilikuwa usiku moja ya njeve, na wale mboch na wadosi wadosi walikuwa wamepoze around nare njo at least wakuwe warm. Pitaa pia alikuwa amedunga poze apo nao akiji warm.
19.Meanwhile, the high priest questioned Jesus about his disciples and his teaching.
Kukiendelea ivo, yule priest sonkwo akauliza JC maswali ju ya mafans wake na teachings zake.

20."I have spoken openly to the world," Jesus replied. "I always taught in synagogues or at the temple, where all the Jews come together. I said nothing in secret.
JC akajibu,"Nimebonga wazi kwa ya world, nimekuwa always nikifundisha kwa ma sinagogue ama kwa temple, place wadhi wote wayahudi hukusanyika tugezza. Sijasema anything kisirisiri.

21.Why question me? Ask those who heard me. Surely they know what I said."
Mbona munaniquestion? Ulizeni wale walinizkiza. For sure wanamesea chenye nilibonga."

22.When Jesus said this, one of the officials nearby struck him in the face. "Is this the way you answer the high priest?" he demanded.
Vile JC aliskia ivo, mmoja wa wale wadosi karibu akamwai kibare ya face. "Hivinjo vile unaweza bonga na high priest?" Akadai kujua.

23."If I said something wrong," Jesus replied, "testify as to what is wrong. But if I spoke the truth, why did you strike me?"
JC akasema, "Ka nimebonga kitu wrong, testifyuseme ni what nimesema iko wrong. Lakini kama nimebonga ukweli, mbona mlinigonga?"

24.Then Annas sent him, still bound, to Caiaphas the high priest.
Kisha Annas akamsend, bado amefungwa, hadi kwa Caiaphas yule high priest.

25.As Simon Peter stood warming himself, he was asked, "You are not one of his disciples, are you?" He denied it, saying, "I am not."
Vile Simon Peter alisimama akijiwarm, aliulizwa niaje, "Si we ni mmoja wa wadhii disciples wake, ama sio?" Pitaa akakwara zi akibonga, "Sio mimi."

26.One of the high priest's servants, a relative of the man whose ear Peter had cut off, challenged him, "Didn't I see you with him in the olive grove?"
Mmoja wa wale mboch wa priest mdosi kabisa, rela wa jamaa alikatwa skio na Pitaa, akamleta juu, "Si nilikucheki na yeye ndani ya ile kichaka ya Olive?"

27.Again Peter denied it, and at that moment a rooster began to crow.
Kisha tena Pitaa akakwara, na iyo time vile likwara tu jogoo akaanza kuwika.

28.Then the Jews led Jesus from Caiaphas to the palace of the Roman governor. By now it was early morning, and to avoid ceremonial uncleanness the Jews did not enter the palace; they wanted to be able to eat the Passover.
Alafu wayahudi wakapeleka JC toka kwa Caiaphas hadi kwa palace ya governor mroman. Kufikia sa hiyo ilikuwa asubuhima ngwarekabisa, na ku avoid ile kujimake religiously unfit for the bash ma jews wakadinda kuingia palace; manzi walitaka kudishi mlo ya passover.

29.So Pilate came out to them and asked, "What charges are you bringing against this man?"
Kisha Pilate akawatokezea pale nje na kuwashow, "Ni charges gani man bring againts huyu jamaa?"
30."If he were not a criminal," they replied, "we would not have handed him over to you."
Wakajibu, "Kama si ati ni jangili, hatungem peana kwenu.

31.Pilate said, "Take him yourselves and judge him by your own law." "But we have no right to execute anyone," the Jews objected.
Pilate akabonga aje, "Mtake-ini nyi wenyewe na mumjugde na constitution yenu." Wayahudi wakateta,"Lakini hatuna rights za ku execute mse yeyote."

32.This happened so that the words Jesus had spoken indicating the kind of death he was going to die would be fulfilled.
Hii ilihappen njo zile words zenye Jesus alikuwa amebonga kushow ni death gani angededi zikuwe fulfilled.

33.Pilate then went back inside the palace, summoned Jesus and asked him, "Are you the king of the Jews?"
Pilate akarudi back hadi ndani ya ile palace, akaita JC na kumwuliza niaje,"We njo yule king wa wayahudi?"
34."Is that your own idea," Jesus asked, "or did others talk to you about me?"
JC akauliza,"Iyo ni idea yako mwenyewe, ama ni wadhii wengine walikuguzia tu ju ya mimi?"
35."Am I a Jew?" Pilate replied. "It was your people and your chief priests who handed you over to me. What is it you have done?"
Pilate aka answer,"Kwani mi ni jew? Ilikuwa ni wadhii wenu na priest mabuda njo walikuleta over kwangu under arrest. Ni nini kwani ume do?"

36.Jesus said, "My kingdom is not of this world. If it were, my servants would fight to prevent my arrest by the Jews. But now my kingdom is from another place."
Jesus akadai, "Kingdom ya mine sio ya hii worlkd. Ka ingekuwa, ma servantswa mine wangetokwa war ku prevent arrest yangu na majews. Lakini sasa kingdom hii ni ya place ingine."

37."You are a king, then!" said Pilate.Jesus answered, "You are right in saying I am a king. In fact, for this reason I was born, and for this I came into the world, to testify to the truth. Everyone on the side of truth listens to me."
"We ni king basi!" Pilate akadai. JC akamjibu, "Uko sawa ukisema atimi ni mfalme. For real, kwanzaju ya hii reason njo maana nilizaliwa, na ju ya hii reason njo nilikam ndani ya world, kutestify ju ya ukweli."Kila mse mwenye ako kwa side ya truth yuu niskizia."

38."What is truth?" Pilate asked. With this he went out again to the Jews and said, "I find no basis for a charge against him.
"Truth ni what sasa?" Pilate akadai. So from hapo akaishia out tena kwa majews na kusema, "Si find reason any nzuri ya a charge against huyu jamaa.

39.But it is your custom for me to release to you one prisoner at the time of the Passover. Do you want me to release 'the king of the Jews'?"
Lakini ni kama kawa ya mimi kurelease kwenu angalau prisoner mmoja izi time za bash ya passover. Mnawant nimrelease'?"

40.They shouted back, "No, not him! Give us Barabbas!" Now Barabbas had taken part in a rebellion.
Waka holla back, "Sio yeye! Tugeini Barabbas!" Sa Barabbas alikuwa ametake partkwa rebellion.

Wednesday, October 7, 2009

John 17

Johnie Chapta ya seventeen-John 17

1.After Jesus said this, he looked toward heaven and prayed: "Father, the time has come. Glorify your Son, that your Son may glorify you.
Baada ya JC kusema ivi, alicheki juu heaven na kupray: "Daddy, time imekam. Glorify son wako,njo son wako aku glorify.

2.For you granted him authority over all people that he might give eternal life to all those you have given him.
Ju umemgei say ju ya wadhi wote njo apeane life ya milele kwa wale wote umempea.

3.Now this is eternal life: that they may know you, the only true God, and Jesus Christ, whom you have sent.
Sa hii njo life ya forever: wakujue, God yule wa ukweli, na Jesus Christ, mwenye umetuma.

4.I have brought you glory on earth by completing the work you gave me to do.
Nishakuletea glory kwa earth vile nimemada works yako yenye ulinigei kufanya.

5.And now, Father, glorify me in your presence with the glory I had with you before the world began.
Na sasa fadhe, niglorify ndani ya presence yako na ile glory nilikuwa nayo na wewe kabla world ianze.

6."I have revealed you to those whom you gave me out of the world. They were yours; you gave them to me and they have obeyed your word.
"Nishakureveal kwa wale wadhi ulinigei toka kwa world. Wao ni wako; uliwagei kwangu na wame obey word yako.
7.Now they know that everything you have given me comes from you.
Sa wanamesea that kila kitu umenigei inakam from wewe.

8.For I gave them the words you gave me and they accepted them. They knew with certainty that I came from you, and they believed that you sent me.
Ju niligeiana kwao words zenye ulinipea na wakazikubali. Walimesea kwa hakika that nimekam from wewe, na wakaamini umenisend.

9.I pray for them. I am not praying for the world,but for those you have given me, for they are yours.
Nawaprayia. Sipray for world, lakini for wale umenigei, ju hao ni wako.

10.All I have is yours, and all you have is mine. And glory has come to me through them.
Kila samo niko nayo ni yako, a kila samo uko nayo ni yangu.Na glory imeshakam kwangu kuwapitia.

11.I will remain in the world no longer, but they are still in the world, and I am coming to you. Holy Father, protect them by the power of your name—the name you gave me—so that they may be one as we are one.
Sitabakia ndani ya world zaidi, lakini wao bado wako ndani ya world, na ninakam kwako. Mbuyuz mholy, waprotect kwa kupitia nguvu za jina yako- jina ulinipea- njo wakuwe one kama tu vile si tuko one.

12.While I was with them, I protected them and kept them safe by that name you gave me. None has been lost except the one doomed to destruction so that Scripture would be fulfilled.
Vile nilikuwa nao, niliwaprotect na kuwaweka safe na jina yako yenye ulinipa. Hanaku hata mmoja mwenye amelost except yule alipangiwa kuwa destroyed njo scripture ikuwe fulfilled.

13."I am coming to you now, but I say these things while I am still in the world, so that they may have the full measure of my joy within them.
Na kam kwako sasa, lakini nasema hizi vitu vile bado niko kwa world, njo sasa wawe na mgawo full ya furaha yangu ndani yao.

14.I have given them your word and the world has hated them, for they are not of the world any more than I am of the world.
Nishawagei word yako na ju ya hiyo world imewahate, ju wao sio wa world kama tu ya vile mimi sio wa world.

15.My prayer is not that you take them out of the world but that you protect them from the evil one.
Prayer ya mine sio that uwachomoe from world lakini that uwa protect from yule mwiked.

16.They are not of the world, even as I am not of it.
Wao sio wa world kama vile pia mimi sio wa world.

17.Sanctify them by the truth; your word is truth.
Waweke set apart by ukweli; word yako ni ukweli.

18.As you sent me into the world, I have sent them into the world.
Vile ulinituma ndani ya world, nimewatuma ndani ya world.

19.For them I sanctify myself, that they too may be truly sanctified.
Kwa sababu yao nimejiseti apart,njo nao pia wakuwe set apart vi thorough.

20."My prayer is not for them alone. I pray also for those who will believe in me through their
message,
"Prayer ya mine sio for wao alone. Naprayia pia wote wenye watabelieve in mimi through message yao,

21.that all of them may be one, Father, just as you are in me and I am in you. May they also be in us so that the world may believe that you have sent me.
that wote watakuwa one, Daddy, kama tu vile we uko in mimi na mimi in wewe. Wacha wao pia wawe ndani yetu njo world i believe that umenituma.

22.I have given them the glory that you gave me, that they may be one as we are one:
nimewagei ile glory that ulinigei, that wao pia wakuwe one kama vile tuko one:

23.I in them and you in me. May they be brought to complete unity to let the world know that you sent me and have loved them even as you have loved me.
Mi in wao na wewe in me. Wacha wabringiwe to complete unity ku let the world ijue that ulinisend na that umewapenda ka tu vile umenipenda.

24."Father, I want those you have given me to be with me where I am, and to see my glory, the glory you have given me because you loved me before the creation of the world.
"Mbuyuz, nataka wale umenigei wakuwe na mimi place niko, na kucheki glory yangu, ile glory umenigei ju ulinipenda kabla ya kucreate the world.

25."Righteous Father, though the world does not know you, I know you, and they know that you have sent me.
" Fadhe mrighteous,ingawa world haikumesei, ninakujua, na wanamesea that ushanisend.

26.I have made you known to them, and will continue to make you known in order that the love you have for me may be in them and that I myself may be in them."
Nishakuintroduce kwao hadi wakakujua, na nitazidi kukufanya ujulikane nao njo love uko nayo kwangu pia ikuwe ndani yao na that mi mwenyewe nikuwe in wao."